You are here
Home > News > Breaking News > The Fearless Mohammed Ali Locks the Bull by It’s Horns, Again!

The Fearless Mohammed Ali Locks the Bull by It’s Horns, Again!

The Fearless Mohammed Ali Locks the Bull by It’s Horns, Again!

Jicho Pevu’s Moha had this to say about his name’s mention by the Interior Security CS Nkaiserry during a security briefing about the Mandera mass grave claim,

“Shikamoo Meja mstaafu Joseph Nkaissery. Natumai u buheri wa afya popote ulipo chini ya ulinzi mkali unaotokana na ushuru wangu na Wakenya wenzangu.

Wiki iliyopita, nilipokuwa nikitazama sherehe za Jamuhuri ya Kenya, twasira yako ilinijia na kutaka kujua ni kwa nini tuwe katika hali ya utumwa tukisheherekea miaka 52 ya uhuru wa taifa hili. Wiki hio hiyo, nikiwa futi kadhaa angani kutoka Mandera, niliarifiwa kuwa ulinitaja jina, sio mara moja, bali mara kadhaa na kuonekana kujaribu kuhusisha jina langu na wanamgambo wa Al-Shabaab, eti nilikuwa nikipasisha ujumbe wao na kutokuwa mzalendo mpenda taifa.

Naarifiwa pia ulitutaka, sijui kama ni mimi na Yassin Juma, tuombe msamaha kwa kutoa taarifa za kutatanisha. Naomba kwa heshima nikuweke sawa mzee wangu. Kwanza kabisa, siombi msamaha maana sijui kosa langu ni lipi. Pili, wa kuomba msamaha ni wewe kwa kutuhusisha sisi wawili na ugaidi ukitumia wadhifa wako, huku ukilegeza kamba kwa kuchagua wanahabari wawili kati ya wote walioripoti tukio hilo.

Je, ulituchagua kwa sababau sisi ni Waisilamu? Je, ulituchagua kwa sababu sisi hatukubaliani na kauli ya serikali? Je, ulituchagua kutokana na msukumo wa wale maskauti wa propaganda 36 wa serikali? Nauliza unijibu.. ”

This is not the first time Mohammed Ali has been at the center of the government’s watchful eyes. But time and time again he stands to speak fearlessly. I wish I had those guts because I have a lot to say.

READ   A Prophet Charges at Lions And Lives to Tell

Leave a Reply

Top